Baada ya Real Madrid na Wolfsburg kusonga mbele na kutinga robo fainali jana usiku, leo vilabu vya Zenit, Benfica, Chelsea na Paris Saint Germain vitakuwa vinawania nafasi ya kufuzu na kuungana na Los Blancos na Wolfsburg.
Mechi ambayo itateka hisia za wadau wengi wa soka duniani ni Chelsea ambao wanaikaribisha PSG pale Stamford Bridge. PSG wakiwa wanaingia dimbani na ushindi wa 2-1 waliopata wiki zilizopita.
Zlatan Ibrahimovic atakuwa anaingia kwenye mchezo akiwa na mission mbili – kuisaidia timu yake kufuzu pamoja na kuingia kwenye listi ya wachezaji 13 ambao wana magoli 50 au zaidi katika michuano ya ulaya.
…read more
Source: Magazetini