MWANZONI mwa mwezi uliopita nyaraka za Panama zilizua taharuki iliyohanikiza dunia nzima zilipoibuka kashfa iliyojitofautisha na kashfa zinazohusisha nchi moja moja. Lundo la nyaraka milioni 11.5 lina taarifa za kampuni zaidi ya laki mbili za ugenini ziliyomo katika orodha ya kampuni za ushauri ya Mossack Fonseca zinazobainisha wamiliki, wenye hisa na viongozi wakuu wa kampuni hizo.
Ni kawaida katika mfumo wa kibiashara kuendesha kampuni nje ya nchi anayotoka mmiliki lakini kisichokuwa cha kawaida kuhusu nyaraka za Panama, ni utajiri wa viongozi mbalimbali duniani ulivyofutikwa usifahamike kwa sababu zinazotia shaka. Awali walitajwa vigogo wachache na ndugu zao lakini baadaye ikadhihirika kuwa visiwa …read more
Source: Magazetini