MOSCOW, URUSI
WAZIRI Mkuu wa Urusi, Dmitry Medvedev amesema vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya taifa hilo ni sawa na kutangaza vita vya kibiashara.
Amesema mikakati iliyotiwa saini na Rais Donald Trump inaonyesha udhaifu wa kiongozi huyo wa Marekani, akisema ameaibishwa na Bunge.
Sheria hiyo inalenga kuiadhibu Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa Marekani wa 2016 pamoja na vitendo vyake dhidi ya Ukraine.
Katika kutia saini makubaliano hayo dhidi ya adui wa Marekani kupitia sheria ya vikwazo siku ya Jumatano, Trump hata hivyo alisema mkakati huo si sawa.
Sheria hiyo pia inaiwekea vikwazo Iran na Korea Kaskazini.
Iran imesema kuwa vikwazo hivyo vipya vinakiuka makubaliano …read more
Source: Magazetini